Uganda kuwa mwenyeji wa mkutano wa 63 wa Jumuiya ya Mashauriano ya Kisheria ya Asia-Afrika
Wawakilishi wa Serikali, wataalam wa sheria, na wajumbe wa kidiplomasia kutoka nchi wanachama 47 wanatarajiwa kukutana nchini Uganda kwa ajili ya mkutano wa 63 wa Jumuiya ya Mashauriano ya Kisheria ya Asia na Afrika (AALCO).
Mwanasheria Mkuu wa Uganda Bw. Kiryowa Kiwanuka amewaambia wanahabari kuwa mkutano huo wa siku tano uliopangwa kuanza Septemba 8, utazingatia maslahi ya nchi wanachama katika sheria za kimataifa na unalenga kueleza mitazamo ya pamoja ya kisheria ya Asia na Afrika katika jukwaa la kimataifa.
Bw. Kiwanuka amesema Jumuiya ya Mashauriano ya Kisheria ya Asia na Afrika inatoa jukwaa kwa nchi wanachama kujadili na kushawishi maendeleo ya sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na sheria ya bahari, mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa mtandao wa Internet, sheria ya biashara ya kimataifa, amani na usalama, na taratibu za kutatua migogoro.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma