

Lugha Nyingine
Kundi la M23 lathibitisha tena ahadi ya kufuata mchakato wa amani
Corneille Nangaa (kushoto), Mkuu wa Kundi la Muungano wa Mto Kongo, ambalo ni shirika la kisiasa na kijeshi linalohusiana na M23, akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Goma, Jimbo la Kivu Kaskazini, DRC, Sepemba 1, 2025. (Str/Xinhua)
Kundi la M23 jana Jumatatu lilithibitisha tena dhamira yake ya kuendeleza mchakato wa amani chini ya upatanishi wa Qatar licha ya tofauti zinazoendelea na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mkuu wa Kundi la Muungano wa Mto Kongo (Congo River Alliance), mshirika wa M23, Bw. Corneille Nangaa akizungumza na wanahabari mjini Goma amesema ana imani na juhudi za upatanishi za Qatar.
Kauli hiyo imetolewa wakati ambapo serikali ya DRC na kundi la M23 yamerejesha mazungumzo huko Doha, ikifuata kanuni zilizosainiwa tarehe 19 Julai ya kupanga kuanzisha mazungumzo kabla ya tarehe 8 Agosti na kufikia makubaliano ya amani ifikapo tarehe 18 Agosti. Licha ya kwamba hatua hiyo haijafikiwa, Doha inasalia kuwa jukwaa pekee la mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili katika wiki za hivi karibuni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma