

Lugha Nyingine
Marufuku ya uvuvi kaskazini mwa China yamalizika baada ya miezi minne
JINAN - Jumatatu mchana mamia ya meli za uvuvi kutoka bandari ya Shidao katika Mkoani Shandong mashariki mwa China, zilifunga safari ya kuelekea baharini, hii imeashiria mwisho wa marufuku ya uvuvi ya miezi kwenye bahari ya Bohai na bahari ya manjano kaskazini mwa latitudo ya nyuzi 35.
Nahodha wa meli moja mvuvi Bw. Zhang Zhiming mwenye umri wa miaka 59, alipoongea na mwandishi wa habari huku akiangalia hali ya hewa na kuwaaga marafiki waliokuwa ufukweni, alisema “Natumai tunaweza kujaza nyavu zetu haraka na kurudi mapema. Tukifanya hivyo, ndivyo tunaweza kuuza samaki kwa bei nzuri na kupata pesa zaidi.”
Mmiliki mwingine wa meli Wang Jie ambaye meli yake inavua samaki aina ya Spanish mackerel alisema, “Kutokana na marufuku ya uvuvi ya msimu, katika miaka ya hivi karibuni ukubwa na ubora wa samaki wanaovuliwa umeongezeka kwa kiasi kikubwa.” Safari moja ya meli yake inaweza kuvua takriban kilo 25,000 hadi 40,000 za samaki.
Ili kurejesha samaki na kuhakikisha uendelevu wake, mwaka 1995 China ilianza kutekeleza marufuku ya uvuvi katika eneo hilo katika majira ya joto. Profesa Xue Ying wa Chuo Kikuu cha Mambo ya bahari ya China, amesema katika miongo mitatu iliyopita, sera hiyo imeongeza kikamilifu idadi ya samaki baharini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma