99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Rais Xi atoa pendekezo la Usimamizi wa Dunia kwenye mkutano mkubwa zaidi wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 02, 2025

Rais Xi Jinping wa China anaongoza Mkutano wa “Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) Plus" na kutoa hotuba yenye kichwa “Kuunganisha Nguvu ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ili Kuboresha Usimamizi wa Dunia” mjini Tianjin, China, Septemba 1, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais Xi Jinping wa China akiongoza Mkutano wa "Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) Plus" na kutoa hotuba yenye kichwa "Kuunganisha Nguvu ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ili Kuboresha Usimamizi wa Dunia" mjini Tianjin, China, Septemba 1, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

TIANJIN -- Rais Xi Jinping wa China Jumatatu alitoa Pendekezo la Usimamizi wa Dunia (GGI), akitoa wito kwa nchi mbalimbali kufanya juhudi za pamoja ili kuanzishwa kwa mfumo wa usimamizi wa dunia wenye haki na usawa zaidi.

Rais Xi amesema hayo wakati akiongoza Mkutano wa "Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) Plus" mjini Tianjin, ambapo jumuiya hiyo imefanya mkutano mkubwa zaidi katika historia yake ya miaka 24, uliohudhuriwa na viongozi kutoka zaidi ya nchi 20 na wakuu wa mashirika 10 ya kimataifa.

Pendekezo la GGI ni pendekezo la nne la Dunia la kihistoria lililotolewa na Xi katika miaka kadhaa iliyopita, kufuatia Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia.

Rais Xi ametaja kanuni tano za Pendekezo la Usimamizi wa dunia (GGI), yaani mamlaka ya nchi kuwa usawa, kufuata sheria za kimataifa, kuutekeleza utaratibu wa pande nyingi, kutetea kipaumbele cha watu, na kuzingatia zaidi kuchukua hatua halisi.

Wakati mwelekeo wa kihistoria wa amani, maendeleo, ushirikiano na kunufaishana ukiwa bado haujabadilika, mawazo ya vita baridi, umwamba na kujilinda kibiashara vinaendelea kuiandama dunia, Rais Xi amesema vitisho na changamoto mpya vimekuwa vikiongezeka, na dunia imejikuta katika kipindi kipya cha misukosuko na mabadiliko, na kusema "usimamizi wa dunia umefika kwenye njia panda mpya."

Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi wa vita vya dunia vya kupinga ufashisti na kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa. Rais Xi amesisitiza kulinda kithabiti hadhi na mamlaka ya Umoja wa Mataifa, na kuhakikisha jukumu lake lisiloweza kuwa na mbadala na umuhimu wake katika usimamizi wa dunia.

Amesema kuwa nchi zote, bila kujali ukubwa, nguvu na utajiri, ni washiriki sawa, watoa maamuzi, na wanufaika katika usimamizi wa dunia. Rais Xi pia amesema kuwa haipaswi kuwa na vigezo viwili, na sheria za ndani za nchi chache hazipaswi kulazimishwa kwa nchi nyingine.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha