99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Serikali ya Ghana yaimarisha usalama katika mkoa wa Savannah ili kutatua mgogoro wa kikabila

(CRI Online) Septemba 01, 2025

Serikali ya Ghana imetoa taarifa ikisema imetuma askari polisi na wanajeshi zaidi katika mkoa wa Savannah nchini humo ili kurejesha utulivu na kusimamisha mapigano ya kikabila kati ya makundi mawili.

Taarifa hiyo imesema waziri wa mambo ya ndani pia ameongoza ujumbe wenye mamlaka ya juu kukutana na viongozi wa makabila ili kujadili hatua za kusimamisha mapigano.

Mapigano makali ya kugombea ardhi kati ya makabila ya Brifo na Gonja yaliyotokea wiki moja iliyopita yamesababisha vifo vya watu 20 na wengine mamia kujeruhiwa, na zaidi 1,000 wamekimbia makazi yao, huku mashamba, maduka na biashara vikitelekezwa au kuharibiwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha