

Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa UM alaani tukio la kukamatwa kwa wafanyakazi wa UM nchini Yemen
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres Jumapili amelaani vikali kukamatwa kiholela kwa wafanyakazi 11 wa umoja huo na kundi la Houthi nchini Yemen mapema siku hiyo katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo.
Bw. Guterres pia amelaani kundi hilo kuingia kwa nguvu katika eneo la kazi la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), unyakuzi wa mali ya Umoja wa Mataifa na majaribio ya kuingia katika maeneo mengine ya kazi ya Umoja wa Mataifa huko Sanaa.
Bw. Guterres ametaka kuachiliwa huru mara moja na bila masharti kwa wafanyakazi hao waliokamatwa pamoja na wengine kutoka umoja huo, mashirika mengine yasiyo ya kiserikali ya kitaifa na kimataifa, asasi za kiraia na ujumbe wa kidiplomasia ambao walikamatwa kiholela tangu Juni mwaka 2024 na wale waliozuiliwa tangu mwaka 2021 na 2023.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma