

Lugha Nyingine
Marekani yakataa kushiriki kwenye duru ya nne ya ukaguzi na majadiliano kuhusu haki za kibinadamu nchini humo
(CRI Online) Agosti 29, 2025
Ujumbe wa kudumu wa Marekani kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva umeambia Ofisi ya Kamishna Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Haki za Binadamu (OHCHR) kuwa, Marekani haitashiriki kwenye duru ya nne ya ukaguzi na majadiliano kuhusu haki za binadamu nchini humo, ambayo yalipanga kufanywa tarehe 6 mwezi Novemba na Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa.
Msemaji wa OHCHR Bi. Ravina Shamdasani jana amethibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, OHCHR imesikitishwa na uamuzi wa Marekani, na itaendelea na mawasiliano na serikali, makundi ya kiraia, wasomi na wafanyabiashara nchini Marekani kuhusu suala la haki za kibinadamu.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma