

Lugha Nyingine
UM: Venezuela haichukuliwi tena kama njia kuu ya kusafirisha dawa za kulevya kwa Marekani na Ulaya
Ripoti mpya ya dawa za kulevya ya dunia ya mwaka 2025 iliyotolewa na Ofisi ya Suala la Dawa za Kulevya na Uhalifu ya Umoja wa Mataifa imetambua Venezuela kuwa nchi isiyo na kilimo haramu cha mihadarati, huku ikisema nchi hiyo haichukuliwi tena kama njia kuu ya usafirishaji wa dawa za kulevya kwa Marekani na Ulaya.
Waziri wa mambo ya ndani, sheria na amani wa Venezuela Bw. Diosdado Cabello amesisitiza kuwa ripoti hiyo imekanusha lawama kuhusu uwepo wa makundi ya wahalifu wa dawa za kulevya nchini Venezuela iliyotolewa na Marekani. Bw. Cabello amelaani tena kuwa Marekani inajaribu kutunga uongo kuhimiza mabadiliko ya utawala wa nchi hiyo.
Waziri huyo amesema, Venezuela inafanya juhudi kuendelea kupambana na usafirishaji wa dawa za kulevya na kufanya operesheni kadhaa za kupambana na dawa za kulevya na kukamata dawa za kulevya zaidi ya tani 50, ikiweka rekodi mpya ya sera za kupiga marufuku ya dawa za kulevya nchini humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma