99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Baraza la usalama la UM lapitisha azimio la kumaliza jukumu la kikosi cha muda cha Umoja huo nchini Lebanon mwishoni mwa 2026

(CRI Online) Agosti 29, 2025

(Picha ilitolewa na Umoja wa Mataifa/kupitia Xinhua)

(Picha ilitolewa na Umoja wa Mataifa/kupitia Xinhua)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kura zote azimio la kurefusha muda wa jukumu la kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL hadi kufikia Desemba 31 mwaka 2026, likianza kuondoa kikosi hicho kwa utaratibu na usalama kuanzia siku hiyo na kumaliza kuondoa askari wote ndani ya mwaka mmoja.

Azimio hilo limetaka kikosi cha UNIFIL kusimamisha operesheni Desemba 31 mwaka 2026, na kuanza kurejesha askari kwa utaratibu na usalama ndani ya mwaka mmoja, huku likiwasiliana na serikali ya Lebanon katika mchakato huo. Lengo la azimio hilo ni kuifanya serikali ya Lebanon kuwa nguvu ya kipekee ya kuhakikisha usalama wa eneo la kusini mwa Lebanon na kutaka katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuripoti maendeleo husika kwa baraza la usalama kila baada ya muda fulani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha