

Lugha Nyingine
Guterres asisitiza UM kuunga mkono Russia na Ukraine kusitisha vita kikamilifu, mara moja na bila masharti
(CRI Online) Agosti 29, 2025
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Stephane Dujarric, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amezungumza na Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine kwa njia ya simu na kusisitiza kuwa Umoja wa Mataifa kuunga mkono usitishaji kamili wa vita, mara moja na bila masharti kati ya Russia na Ukraine.
Bw. Guterres amesisitiza kuwa hiyo ni hatua ya kwanza kuelekea amani ya haki, pana na endelevu nchini Ukraine, kwa mujibu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa, sheria za kimataifa na maazimio husika ya Umoja wa Mataifa.
Msemaji huyo amesema Bw. Guterres pia amesisitiza ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kuendelea kushughulikia mahitaji ya kibinadamu ya Ukraine na kuunga mkono juhudi zake za kurejesha na kujenga upya.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma