

Lugha Nyingine
Milingoti ya taa katika mji wa Shenzhen kusini mwa China yabeba kiota kizuri kwa ndege
Picha hii iliyopigwa tarehe 25 Mei 2024 inaonyesha vifaranga wa ndege aina ya magpie robin kwenye "taa za kiota cha ndege" katika bustani ya ikolojia ya mikoko ya Futian huko Shenzhen, Mkoani Guangdong China. (Xinhua)
SHENZHEN – Jua linapozama mjini Shenzhen mkoani Guangdong China , mwanga usio wa kawaida unatanda kwenye bustani ya ikolojia ya mikoko ya Futian mjini humo, ambapo nguzo 100 za taa zinatoa mwanga mdogo na kila moja inakuwa ni kiota cha ndege.
Mabadiliko haya ambayo hayakupatikana kirahisi, yalianza katika majira ya mchipuko mwaka 2020. Zamani, mlinzi wa bustani Bw. Rong Canzhong aliona ndege mmoja mkubwa akijenga kiota kwenye tundu la nguzo ya taa, na baadaye yeye na wenzake waligundua viota kwenye taa 14. Bw. Rong alisema, “ndege wanaojenga viota kwenye matundu ya nguzo kwasababu hawawezi kuchimba mashimo ya viota vyao wenyewe.” Lakini ni mara chache miti ya mijini kuweza kuwa na matundu ya asili, na hivyo milingoti ya taa inakuwa kimbilio lao. Hata hivyo mpango huo wa muda una hatari, kwani viota vinaweza kuanguka, na maji yakipenya yanaweza kuhatarisha mifumo ya umeme.
Badala ya kuwafukuza ndege hao, timu ya Bw. Rong ilianza kupanga pamoja maeneo salama kwa ajili ya ndege hao, huku wakizingatia utoaji mwanga na uhai wa ndege.
Utafiti wao wa mwaka mzima ulileta utatuzi wa busara, uliopatiwa hakimiliki mwaka wa 2023. Bustani hiyo ilibadilisha taa za kawaida, na sasa ina jumla ya "taa za kiota cha ndege" 100 maalum, zikiwa kwenye milingoti 40 ambayo ina masanduku ya viota vinavyoweza kuondolewa ili kuzuia kuanguka. Balbu zimechaguliwa kwa uangalifu ili kuepuka mwanga wenye mawimbi yanayoweza kuwadhuru wadudu wanaruka.
Bw. Rong amesema viota 75 vimesaidia kuimarisha maisha ya ndege katika miaka mitano iliyopita. Kutokana na kamera zilizofichwa ambazo zinafuatilia halijoto na unyevu, hata mabadiliko kidogo sana ya hewa kwenye kila kiota cha ndege, sasa zinaleta kielelezo kwa miundo ya baadaye ya makazi yao mijini katika kituo cha ikolojia cha Chuo Kikuu cha Sun Yat-sen.
Viota hivi vya mijini sio tu ni matokeo ya uvumbuzi wa kienyeji, bali pia ni sehemu ya matarajio mapana ya Shenzhen kama kituo muhimu kwenye Njia ya kuhamahama kwa ndege ya Asia mashariki-Australasia. Wakati wa majira ya uhamiaji, bustani hupunguza mwanga wa taa ifikapo saa 11 jioni, ili ndege wapumzike bila usumbufu.
Maendeleo yanaweza kupimika, hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu, aina 429 za ndege walikuwa wameishi mjini Shenzhen, ikiwa ni pamoja na aina 15 zinazolindwa. Kwa sasa uhifadhi wa ndege umewekwa wazi kwenye mpango mpya wa ulinzi wa wanyamapori wa mji huo.
Picha hii iliyopigwa tarehe 25 Mei 2024 inaonyesha “kiota chenye mwanga” kwenye bustani ya ikolojia ya mikoko ya Futian huko Shenzhen, Mkoani Guangdong China. (Xinhua)
Uwekaji wa nguzo za chuma kwenye Daraja la Mto Hanjiang la reli ya kasi ya Xi'an-Shiyan wakamilika
Michezo ya Dunia ya Chengdu | Sherehe ya Kufungwa kwa Michezo ya 12 ya Dunia yafanyika
Reli ya kasi China iliyoko kaskazini zaidi mwa China yafikisha miaka 10 tangu ilipoanzishwa
Mandhari ya Arxan yenye vivutio vingi vya utalii, Kaskazini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma