99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa atoa wito wa kulinda utaratibu wa kimataifa wa bahari

(CRI Online) Agosti 12, 2025

Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong ametoa wito wa kulinda utaratibu wa kimataifa wa bahari unaozingatia sheria ya kimataifa katika mjadala wazi wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja huo kuhusu suala la usalama baharini uliofanyika jana tarehe 11.

Balozi Fu amesema Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Bahari ni nyaraka za kisheria jumuishi zinazohusu sekta ya baharini, ikiwa nguzo ya utaratibu wa kisasa wa bahari pamoja na mikataba mingine ya kimataifa na sheria za kimila za kimataifa. Pande husika zinahitaji kuutumia kwa usahihi Mkataba huo kama ipasavyo, kuboresha mawasiliano katika migogoro, kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kuitatua kwa njia ya amani.

Balozi huyu pia amesema China ikiwa ni nchi kubwa inayoendelea ya bahari, inatekeleza kikamilifu majumuku yake yaliyokubaliwa katika Mkataba huo, na itaendelea kutoa huduma mbalimbali za umma za baharini kwa jumuiya ya kimataifa na kushirikiana na nchi mbalimbali duniani kufanya juhudi kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya mambo ya bahari.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha