

Lugha Nyingine
Kusonga Mbele – Kipindi cha 5: Ahadi ya Kufanika
"Kusonga Mbele: Ahadi ya Kufanikiwa" ni sehemu ya tano ya mfululizo wa filamu kuhusu simulizi na moyo wa askari wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) wanaotekeleza majukumu waliyopewa na Chama na wananchi.
Filamu hiyo inaonyesha uvumbuzi wa jeshi la PLA katika nyanja mbalimbali za kupigana vita. Kutoka ndege ya usafirishaji wa kimkakati wa Y-20 inayoweza kuhamasisha kwa haraka hadi kikosi cha makombora cha kuweza kulenga mashabaha kwa usahihi, na kutoka kikosi cha kwanza cha manowari cha kubeba ndege cha China kinachoonesha uwezo wa kupigana vita kwa pamoja kwa jeshi la anga na jeshi la majini, hadi manowari ya kisasa ya kuendeshwa kwenye maji na barani zinazofanya mazoezi ya pamoja ya kupanda pwani, hayo yote kwa pamoja yameonesha maendeleo ya teknolojia na ahadi ya kufanikisha ya jeshi la PLA katika kuendeleza uwezo wa kupigana vita kwenye mfumo wa mambo ya kisasa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma