

Lugha Nyingine
UNESCO yazindua safari ya Mlima Kilimanjaro ili kuongeza uelewa wa kuyeyuka kwa barafu
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) imesema, safari ya watu 50 kupanda Mlima Kilimanjaro inaendelea ili kuongeza uelewa kuhusu kuyeyuka kwa haraka kwa barafu kunakosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Mlima Kilimanjaro, ambao umewekwa katika Orodha ya Urithi wa Dunia tangu mwaka 1987 na chanzo muhimu cha maji kwa mamilioni ya Wakenya na Watanzania, unapoteza barafu yake kwa kasi kubwa.
Vijana kutoka Kenya, Tanzania, Marekani, wanasayansi, wataalamu wa Umoja wa Mataifa, na wanaharakati wa mazingira wameanza kupanda mlima huo Jumatatu wiki hii, ili kuelekeza macho ya jamii ya kimataifa kuhusu tishio hilo.
UNESCO imesema, tangu mwaka 1912, Mlima Kilimanjaro umepoteza asilimia 85 ya barafu yake na zaidi ya asilimia 30 ya msitu wake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma