

Lugha Nyingine
Wapalestina 83 wauawa kwenye mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza
(CRI Online) Agosti 06, 2025
Taasisi ya Ulinzi wa Raia ya Ukanda wa Gaza jana imesema, wapalestina 83 wameuawa katika shambulizi la risasi na mizinga lililofanywa na Israel dhidi ya Gaza Jumanne.
Msemaji wa Taasisi hiyo, Mahmoud Basal, amesema miongoni mwa waliouawa ni watu 58 waliokuwa wakisubiri misaada katika maeneo ya kaskazini, kati na kusini mwa Gaza.
Ameongeza kuwa hospitali za Gaza zilipokea majeruhi wengi kutokana na mashambulizi ya Israel.
Hakuna taarifa zozote zilizotolewa na jeshi la Israel kuhusu matukio hayo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma