Kamati Kuu ya 20 ya CPC kufanya mkutano wa nne wa wajumbe wote mwezi Oktoba
BEIJING – Mkutano wa nne wa Wajumbe Wote wa kamati kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umepangwa kufanyika Beijing mwezi Oktoba, kwa mujibu wa uamuzi uliotolewa katika kikao cha Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC jana Jumatano ambacho kiliongozwa na Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC.
Kwa mujibu wa ajenda kuu za mkutano huo, Ofisi ya Siasa itatoa ripoti ya kazi yake kwa Kamati Kuu ya CPC, na mkutano huo utajadili mapendekezo ya kuandaa Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii ya Miaka Mitano (2026-2030).
Kikao hicho cha Jumatano, pia kilichambua na kujadili hali ya uchumi ya hivi sasa na kufanya mipango kwa kazi za kiuchumi katika nusu ya pili ya mwaka huu.
Kikao hicho kimedhihirisha kuwa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano ni kipindi muhimu cha kuimarisha msingi na kufanya juhudi kwa pande zote kwa ajili ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya kijamaa.
"Maendeleo ya China yanakabiliwa na mabadiliko na changamano kubwa, kwani fursa, hatari na changamoto za kimkakati vinatokea sanjari na hali ya kutokuwa na uhakika na mambo yasiyotarajiwa yanaongezeka" kikao hicho kimesema.
"Wakati huo huo, msingi wa uchumi wa nchi umeimarishwa, kuna nguvu bora mbalimbali, uhimilivu mkubwa, na uwezo mkubwa, na nguzo za kutegemeka na mwelekeo wa kimsingi kwa ajili ya maendeleo mazuri ya kiuchumi ya muda mrefu havijabadilika," kikao hicho kimesema, kikiongeza kuwa, nguvu za ujamaa wenye umaalum wa China na vile vile soko kubwa la nchi hiyo, mfumo kamili wa viwanda na rasilimali nyingi za vipaji zinazidi kuongezeka.
Kikao hicho kimesema ili kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii katika kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano, China itatekeleza kikamilifu kwa makini wazo jipya la maendeleo, kushikilia kusonga mbele kwa hatua madhubuti, na kuharakisha kuanzisha hali mpya ya maendeleo.
Kimesema kuwa katika kipindi hicho, China itaendelea kuwianisha maendeleo na usalama, kuboresha ipasavyo na kupanua kwa kufaa ukubwa wa uchumi, kusukuma mbele maendeleo ya watu katika mambo yote, na kupiga hatua madhubuti kuelekea ustawi wa pamoja, ili kuhakikisha maendeleo ya lazima yanapatikana katika kutimiza kimsingi ujenzi wa mambo ya kisasa ya kijamaa.
Mandhari ya Kipekee ya Karst katika Mkoa wa Guizhou yavutia watalii
Tamasha la kimataifa la densi lafunguliwa katika Mkoa wa Xinjiang, China likiwa na maonyesho 52
Wakulima wa China wawa na pilikapilika za uzalishaji wa kilimo katika kipindi cha Dashu
Maliasili nyingi za chumvi zaongeza mapato ya wanakijiji katika Wilaya ya Gegye, Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma