

Lugha Nyingine
CCTV kurusha mfululizo wa vipindi juu ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) kuanzia Agosti Mosi
Mfululizo wa vipindi vitano vya TV, "Kusonga Mbele" (Forging ahead), vimepangwa kuanza kuonyeshwa kwenye Televisheni Kuu ya China (China Central Television, CCTV), ambayo ni shirika la utangazaji la Serikali ya China, Ijumaa wiki hii, Agosti Mosi, ukiadhimisha miaka 98 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA).
Vikiwa vimeandaliwa na Idara ya Kazi ya Kisiasa chini ya Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), Ofisi ya Kamati Kuu ya Mambo ya Mtandao ya China, na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG), mfululizo huo wa vipindi vinaangazia simulizi na ari ya askari wa PLA katika juhudi zao za kutimiza majukumu waliyokabidhiwa na Chama na wananchi. Leo Alhamisi, trela imetolewa kwa umma. Tazama matukio ya kusisimua na tenga muda wako kwa ajili ya "Kusonga Mbele".
Mandhari ya Kipekee ya Karst katika Mkoa wa Guizhou yavutia watalii
Tamasha la kimataifa la densi lafunguliwa katika Mkoa wa Xinjiang, China likiwa na maonyesho 52
Wakulima wa China wawa na pilikapilika za uzalishaji wa kilimo katika kipindi cha Dashu
Maliasili nyingi za chumvi zaongeza mapato ya wanakijiji katika Wilaya ya Gegye, Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma