

Lugha Nyingine
Kenya kuwa mwenyeji wa maonesho ya kilimo ili kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya China na Afrika
Kenya imepangwa kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Afrika (AIAE) 2025 mwezi Oktoba, yakilenga kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika biashara ya kilimo na uwekezaji, waandaaji wa maonyesho hayo wamesema jana Jumanne.
Maonesho hayo yaliyopangwa kufanyika Oktoba 28 hadi 31, yameandaliwa kwa pamoja na Maonesho ya Kimataifa ya Hunan Hongxing na Maonesho ya Kilimo Afrika, kwa uungaji mkono wa Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo ya Kenya na yatafanyika chini ya kaulimbiu "Kuongeza Tija ya Kilimo Barani Afrika Kupitia Uvumbuzi na Ufikiaji wa Soko".
Akizungumza na wanahabari katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo ya Kenya, Paul Kipronoh Ronoh, amesema maonesho hayo yatatoa jukwaa kwa wadau wa Afrika kujaribu na kufahamu teknolojia za kisasa kutoka China na dunia nzima zinazohitajika kuifanya sekta ya chakula katika bara hilo kuwa ya kisasa.
Kwa mujibu wa Ronoh wageni zaidi ya 15,000 wanatarajiwa kushiriki maonesho hayo.
Naye Ding Guiping, naibu meneja mkuu wa Maonesho ya Kimataifa ya Hunan Hongxing, amesema maonesho hayo ya mwaka huu yatavutia ushiriki wa nchi 17 na waonyeshaji wapatao 200, zikiwemo kampuni 100 za China.
Mandhari ya Kipekee ya Karst katika Mkoa wa Guizhou yavutia watalii
Tamasha la kimataifa la densi lafunguliwa katika Mkoa wa Xinjiang, China likiwa na maonyesho 52
Wakulima wa China wawa na pilikapilika za uzalishaji wa kilimo katika kipindi cha Dashu
Maliasili nyingi za chumvi zaongeza mapato ya wanakijiji katika Wilaya ya Gegye, Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma