99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Naibu Waziri Mkuu wa China ahimiza juhudi za kulinda maisha na mali za watu walioathiriwa na mafuriko

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 30, 2025

Naibu Waziri Mkuu wa China Zhang Guoqing, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC),  akimpa pole mgonjwa katika hospitali moja ya Eneo la Miyun la Beijing, mji mkuu wa China, Julai 28, 2025. (Xinhua/Liu Bin)

BEIJING – Naibu Waziri Mkuu wa China Zhang Guoqing aliwasili katika Eneo la Miyun la Beijing, jana Jumatatu jioni kutembelea na kufariji wakazi waliolazimika kuhama makazi yao kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, na pia alisimamia kazi za kudhibiti mafuriko na kutoa msaada huko.

Zhang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), alitembelea hospitali, makazi ya muda na Bwawa la Kuhifadhi Maji la Miyun, akiwa amekabidhiwa na jukumu hilo na Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC.

Amewasilisha ufuatiliaji wa Rais Xi, na kufahamishwa kwa makini kuhusu kazi za utafutaji na uokoaji wa waathirika, utoaji huduma za matibabu, uhamishaji watu na miradi ya kudhibiti mafuriko.

Zhang akisema kuwa, hivi sasa China iko katika kipindi muhimu cha kudhibiti mafuriko, na ametoa wito wa kutathmini kwa pande zote hali ya kutokuwa na uhakika kuhusu kutolewa kwa maji kutoka sehemu ya juu na kuelekea sehemu ya chini, pamoja na usalama wa mabwaya ya kuhifadhi maji.

"Ratiba za kufungulia na kuchepusha maji zinapaswa kutekelezwa kwa usahihi kwa njia ya kisayansi ili kupunguza hasara," amesema.

Zhang ametoa wito wa kuboreshwa kwa mifumo ya ufuatiliaji na utoaji tahadhari, ili kuamua mapema kuhamisha watu watakaoathiriwa, akisisitiza kuwa, ni lazima kufuatilia kwanza makundi ya watu wenye hali dhaifu kama vile wazee na watu wenye taabu ya kutembea ili kuhakikisha kila mtu anahamishwa salama.

Operesheni za kutoa msaada na uokoaji kwa nguvu zote zinaendelea Beijing, kwani dhoruba kubwa za mvua za hivi punde zimesababisha vifo vya watu 30 katika mji mkuu huo wa China hadi kufikia saa sita usiku Jumatatu, barabara zimeharibiwa, umeme umekatika na watu wengi wanalazimika kuhama kutoka kwenye sehemu zilizoathirika.

Naibu Waziri Mkuu wa China Zhang Guoqing, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitembelea Bwawa la Kuhifadhi Maji la Miyun  katika Eneo la Miyun la Beijing, Julai 28, 2025. (Xinhua/Liu Bin)

Naibu Waziri Mkuu wa China Zhang Guoqing, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitembelea makazi ya muda katika Eneo la Miyun la Beijing, Julai 28, 2025. (Xinhua/Liu Bin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha