99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

SADC yahimizwa kufanyia tathmini upya uhusiano wa kibiashara kufuatia ushuru uliowekwa na Marekani

(CRI Online) Juni 06, 2025

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Elias Magosi amesema, Jumuiya hiyo inapaswa kutathmini tena uhusiano wake wa kibiashara ili kuongeza manufaa zaidi katika kukabiliana na kuongezeka kwa ushuru wa biashara wa Marekani na kuondolewa uungaji mkono wa maendeleo.

Bw. Magosi amesema hayo katika Mkutano wa 34 wa Kamati ya Mawaziri wa Biashara na Mkutano wa 24 wa Kikosi Kazi kuhusu Mafungamano ya Kiuchumi ya Kikanda iliyofanyika katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.

Amesema mazingira ya ushuru kimataifa yanayobadilika yameunda upya mienendo ya biashara, ikiifanya kanda hiyo kuchukua hatua za mwitikio za kivitendo na kimkakati.

Amesema nchi nyingi wanachama wa SADC zilizowahi kunufaika na Mpango wa Ukuzaji Fursa za Kiuchumi Afrika (AGOA), ziko hatarini kuathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na ongezeko la ushuru wa asilimia 10 ambao Marekani inafikiria kuweka katika bidhaa zote zinazoagizwa kutoka nje.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha