99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Uganda kuwa mwenyeji wa mkutano kilele wa amani na usalama wa kikanda

(CRI Online) Mei 28, 2025

Mawaziri wa Afrika wanakutana nchini Uganda kabla ya mkutano wa kilele wa kikanda kuhusu amani na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na eneo la Maziwa Makuu, unaotarajiwa kufanyika leo Jumatano.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imetangaza Jumanne kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa 12 wa Ngazi ya Juu wa Mfumo wa Uangalizi wa Kikanda wa Mwongozo wa Amani, Usalama, na Ushirikiano (PSC) kwa DRC na eneo la Maziwa Makuu.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, mkutano huo unaohudhuriwa na mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi wanachama, utaangazia sababu za kimuundo za kukosekana kwa utulivu na migogoro kujirudiaa mara kwa mara mashariki mwa DRC na eneo la Maziwa Makuu.

Nchi 11 katika kanda hiyo zilitia saini Mwongozo wa PSC mwaka 2013, zikiahidi kuchukua hatua za kitaifa, kikanda, na kimataifa za kuimarisha amani na usalama mashariki mwa DRC na kuongeza ushirikiano wa kiserikali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha