99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Kenya yafuta ratiba ya kufungua Ofisi ya Mawasiliano ya Somaliland mjini Nairobi

(CRI Online) Mei 28, 2025

Kenya imefuta ratiba ya kufungua ofisi ya mawasiliano mjini Nairobi juzi Jumatatu, tukio lililokuwa limepangwa kufanywa jana Jumanne na Jimbo la Somaliland nchini Somalia, ikisema kuwa tukio hilo halijapata idhini rasmi.

Katika taarifa iliyotolewa mjini Nairobi, Wizara ya Masuala ya Kigeni na Diaspora ya Kenya imesema, Kenya inadumisha na kuthibitisha kwa heshima bila kuyumba utambuzi wake wa Jamhuri ya Muungano wa Somalia kama nchi huru.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Kenya inathamini uhusiano wake na Somaliland, ambayo haijatambuliwa kimataifa, na serikali nyingine za kikanda, kwa lengo la kuhimiza amani, usalama, biashara na uwekezaji katika eneo hilo.

Hata hivyo, wizara hiyo imesema kuwa bado iko wazi kuhakiki ombi la Somaliland kufungua ofisi ya mawasiliano jijini Nairobi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha