99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yaendelea kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika

(CRI Online) Mei 21, 2025

Msaidizi wa Waziri wa Biashara wa China Tang Wenhong amesema, mwaka jana thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola bilioni 295.6 za Kimarekani, ongezeko la asilimia 4.8 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia, na kuvunja rekodi kwa miaka 4 mfululizo.

Amesema, China imeendelea kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Bara la Afrika kwa miaka 16 mfululizo.

Tang ametoa kauli hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu Maonesho ya nne ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika.

Maonyesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 12 hadi 15 mwezi ujao mjini Changsha, China, na hadi sasa zaidi ya watu elfu 12 kutoka nchi 44 za Afrika, mashirika 6 ya kimataifa, mikoa na miji 23 ya China, na zaidi ya mashirika 2,800 ya China na Afrika wamejiandikisha kuhudhuria maonesho hayo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha