99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Msumbiji yapata tuzo kwa maendeleo katika udhibiti wa malaria

(CRI Online) Mei 20, 2025

Ofisi ya Rais wa Msumbiji imetangaza kuwa Msumbiji imepata tuzo ya kupambana na ugonjwa wa malaria iliyotolewa kwenye mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani (WHA) unaofanyika mjini Geneva, ambapo waziri wa afya wa nchi hiyo Bw. Ussene Isse amepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Msumbiji.

Tuzo hiyo imeonesha juhudi za Msumbiji katika kuzuia malaria, ikiwa ni pamoja na usambazaji wa vyandarua kwa watu wengi, kampeni za unyunyiziaji wa dawa ndani, kuboresha huduma za uchunguzi, na kuimarisha ufuatiliaji wa wagonjwa.

Maofisa wa serikali wamesema kuwa tuzo hiyo itaimarisha juhudi za Msumbiji za kutokomeza ugonjwa wa malaria na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, na inalenga kuhakikisha ugonjwa huo hauwi tishio tena kwa afya ya umma nchini Msumbiji na duniani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha