99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Usafirishaji wa mizigo kwa treni ya SGR ya Kenya waongezeka kwa asilimia 40 katika robo ya kwanza ya mwaka

(CRI Online) Mei 15, 2025

Shirika la Reli la Kenya (KRC) limesema katika ripoti iliyotolewa jana Jumatano kuwa, mahitaji ya huduma ya usafirishaji wa mizigo ya Reli ya SGR nchini Kenya yameongezeka kwa asilimia 40 katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

Ripoti hiyo pia imesema, reli ya SGR ilisafirisha tani milioni 1.82 za mizigo katika kipindi cha miezi mitatu, kutoka tani milioni 1.3 katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Aidha, mapato kutokana na huduma ya usafiri wa abiria yalipanda hadi shilingi bilioni 3.82 za Kenya (sawa na dola za kimarekani milioni 29.5) katika kipindi hicho, kutoka dola milioni 25 mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha