99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Spika wa Bunge la China afanya mazungumzo na mwenzake wa Zimbabwe mjini Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 14, 2025

Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akifanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Zimbabwe Jacob Mudenda kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Mei 13, 2025. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BAEIJING - Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Zimbabwe Jacob Mudenda mjini Beijing jana Jumanne, akisema kwamba tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Zimbabwe miaka 45 iliyopita, nchi hizo mbili zimekuwa zikiaminiana na kuungana mkono wakati wote, na uhusiano Kati ya pande mbili umestahimili majaribu ya wakati na mabadiliko katika hali ya kimataifa.

Zhao, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China amesema wakuu wa nchi hizo mbili walifanya mazungumzo ya kina, ya kirafiki mjini Beijing mwaka jana na kufikia maafikiano muhimu, wakiweka dira ya maendeleo ya uhusiano na ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande mbili.

Amesema China inapenda kushirikiana na Zimbabwe kutekeleza makubaliano hayo yaliyofikiwa kati ya marais wao wawili na kujenga jumuiya ya China na Zimbabwe yenye mustakabali wa pamoja yenye kiwango cha juu.

Zhao amesema, China inapenda kufanya juhudi za pamoja na Zimbabwe kudumisha na kuendeleza hali ya juu ya kuaminiana kisiasa kati ya nchi hizo mbili na pia inapenda kuendelea kuungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi ya msingi ya kila mmoja, kuimarisha muunganisho wa mikakati ya maendeleo, na kuongeza uratibu wa kimataifa.

“China inakaribisha wabunge wa Zimbabwe kuja China kufanya mawasiliano na ziara zaidi,” Zhao ameongeza.

Ameeleza kuwa, Bunge la China linapenda kubadilishana uzoefu na Zimbabwe kuhusu kuimarisha utawala wa kisheria katika maeneo kama vile ujenzi wa maeneo maalum ya kiuchumi na upanuzi wa maeneo ya ufunguaji mlango, na inakaribisha Zimbabwe kushiriki katika mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalum wa China na kunufaishwa na fursa zake za maendeleo.

Kwa upande wake Mudenda amesema kuwa chini ya uongozi wa marais hao wawili, ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya Zimbabwe na China umeimarishwa, na kwamba Zimbabwe inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na inaishukuru serikali ya China na watu wakea kwa uungaji wao mkono muhimu wa muda mrefu.

“Zimbabwe inapenda kuimarisha ushirikiano wa kivitendo na China katika maeneo kama vile biashara, nishati, kilimo, akili bandia na utamaduni” amesema.

Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akifanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Zimbabwe Jacob Mudenda kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Mei 13, 2025. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akifanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Zimbabwe Jacob Mudenda kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Mei 13, 2025. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha