99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Kenya kuongeza mauzo ya chai yake nchini China

(CRI Online) Mei 13, 2025

Kenya inalenga kuongeza mauzo ya chai yake nchini China kwa zaidi ya mara nne katika miaka sita ijayo.

Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo wa Kenya, Mutahi Kagwe amesema, lengo ni kuongeza mauzo hayo ya chai ya Kenya nchini China kutoka kilogramu milioni 12.42 za mwaka 2024 hadi kilogramu milioni 50 itakapofika mwaka 2030.

Waziri Kagwe amesema hayo katika taarifa iliyotolewa jijini Nairobi, baada ya kukutana na Zhang Chaobin, mwenyekiti wa Kampuni ya Chai ya Benny ya mkoani Fuzhou, China.

Kagwe amesema mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kuongeza uwepo wa Kenya katika soko la chai la China, akiongeza kuwa, mawasiliano hayo ya ngazi ya juu yanaonyesha mkakati wa Kenya wa kuboresha mauzo yake ya chai ya kipekee nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha